Waziri
wa Fedha Zanzibar Mhe. Omar Yusuf Mzee akifungua pazia kuashiria
ufunguzi wa kituo cha utabibu na uzalishaji mifugo kiliopo Mangapwani
Mkoa Kaskazini `B’ Unguja.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Kasim Gharib Juma akitoa maelezo
ya kituo cha utabibu na uzalishaji mifugo kiliopo Mangapwani Mkoa
Kaskazini `B’ Unguja
Waziri
wa Fedha Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee akizungumza na wananchi katika
ufunguzi wa kituo cha utabibu na uzalishaji mifugo. Kulia ni Katibu
Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Kasim Gharib na kushoto Mkuu wa Mkoa
Kaskazini Unguja Pembe Juma Khamis.
Baadhi
ya wananchi waliohudhuria katika ufunguzi wa kituo cha utabibu na
uzalishaji mifugo Mangapwani Mkoa Kaskazini `B’ Unguja wakimsikiliza
Waziri wa Fedha Mh. Yussuf Omar Mzee( hayupo pichani).Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
---
Na Ali Issa na Miza Othman Maelezo –Zanzibar. 5/12/013
Waziri
wa Fedha wa Zanzibar Mh. Omar Yussuf Mzee ameitaka Wizara ya Mifugo na
Uvuvi kuwashajihisha wananchi wa Mangapwani na vitongoji vyake
kukitumia kituo cha utababu na uzalishaji mifugo kilichopo Mangapwani
Wilaya ya Kaskazini B kupeleka mifugo yao kwa ajili ya kupatiwa
matibabu na kupata mbegu bora za mifugo.
Hayo
ameyasema leo huko Mangapwani wakati wa uzinduzi wa kituo cha utabibu
wa mifugo kijijini hapo ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kutimiza
miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema
kwa muda mrefu wafugaji wamekua wakipata usumbufu wa kufuata huduma za
mifugo mbali na eneo hilo hivyo utanuzi wa vituo vya utibabu na
uzalisha mifugo vijijini ni kuwapunguziamatatizo wananchi na
amewashauri kuvitumia ili kuongeza uzalishaji wa mifugo.
“Ili
kufikia lengo la kuwepo kwa kituo hiki hapa ni kwa wananchi kukitumia
kikamilifu kupeleka mifugo yao kupatiwa matibabu, mbegu bora za mifugo
na ushauri kutoka kwa watalamu wa mifugo”, alisema Waziri .
Aliongeza
kuwa katika kufanikisha hatua hiyo Wizara ya Mifugo italazimika kutoa
elimu ya kutosha kwa wafugaji kukitumia kituo hicho kupata matibabu
ya mifugo yao pamaoja na kupatiwa mbegu bora za kisasa za mifugo
itakayowapatia tija kwa haraka.
Alidokeza
kuwa kabla ya Mapinduzi ya 1964 kituo cha utabibu wa mifugo kilikuwa
kimoja tu kwa Unguja katika eneo la Maruhubi ambacho kilitoa huduma kwa
wafugaji wote lakini kupelekwa huduma hiyo karibu na wananchi vijini ni
frusa pana kwa wafugaji kuongeza uzalishaji.
Nae
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Pembe Juma Khamiss akimkaribisha
Waziri huyo aliiomba Wiraza pamoja na kituo hicho kujenga majosho ya
kuoshea mifugo pamoja na kupeleka madaktari wa mifugo kituoni hapo.
Aidha
alisema hadi hivi sasa Mkoa wake umepata vituo viwili vinavyotoa
huduma za Afya ya mifugo jambo linaloleta faraja kubwa kwa wananchi
kwani ndio mkoa unaoongoza kwa wafugaji wengi.
Mapema
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kassim Gharibu amesema Wizara
ya Uvuvi na Mifugo inawataalamu wakutosha wa afya ya mifugo jambo
ambalo litawezesha vituo vyote vitakavyoanzishwa kutoa huduma kwa
ufanisi bila matatizo yoyote.
Alisema
Wizara imejipanga vizuri kusambaza vituo vya huduma za mifugo Unguja
na Pemba na mpaka sasa imeshajenga vituo 23, Unguja 12 na Pemba 11.
Ujenzi wa kituo hicho umefadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la IFAD na kimegharimu Shilingi milioni 22 za kitanzania.
No comments:
Post a Comment