Thursday, December 5, 2013

Nchimbi abebeshwa zigo la Prof Kapuya


WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi ameingia lawamani kwa kudaiwa kumlinda Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), anayedaiwa kumbaka na kumtishia kumuua binti wa miaka 16.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.
Akizungumza kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi wa simu (sms) na Tanzania Daima jana, binti anayelalamika kutishiwa maisha na Profesa Kapuya, amemtuhumu Waziri Nchimbi kushindwa kulishughulikia suala hilo mapema licha ya kuwa na taarifa za tukio hilo muda mrefu.
Binti huyo alisema kuwa Dk. Nchimbi ni miongoni mwa mawaziri na viongozi wa CCM waliokuwa wakifahamu kila kinachoendelea dhidi ya malalamiko husika.
Alibainisha kuwa makada hao wa CCM walikuwa wakifanya jitihada za kuhakikisha manyanyaso na vitisho kutoka kwa Profesa Kapuya haviwekwi hadharani.
Katika kile kinachoonekana ni kukata tamaa juu ya usalama wake pamoja na dada yake, binti huyo alisema amewasiliana na Waziri Nchimbi asubuhi ya jana na kwamba waziri huyo hakuonyesha dalili yoyote ya kujali madhila yao.
Alisema kutokana na Waziri Nchimbi kutokutilia uzito malalamiko yao, waliamua kumuandikia ujumbe mfupi wa maandishi wakimshutumu kuendelea kumlinda Profesa Kapuya.
“Nimemwambia katika ujumbe mfupi wa maneno (sms) kuwa jukumu la polisi iliyo chini ya wizara yake ni kuhakikisha wananchi wanalindwa dhidi ya manyanyaso na vitisho vya aina yoyote, na kwamba katika kadhia hii ya Kapuya Jeshi la Polisi limekuwa kimya.

No comments:

Post a Comment