Monday, December 9, 2013

Taswira:Umati wa Wananchi Wajitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt.Wilbrod Slaa Mjini Kasulu,Vijana wapatao 10-15 Wajitokeza na Mabango Wananchi Wawafukuza kwa kitendo cha kuvamia mkutano wa chadema na kupiga kelele ili mkutano usiendelee.

 Sehemu ya Mabango yaliyobebwa a Vijana wapatao 10-15
 Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akihutubia katika Mkutano uliofanyika  Kasulu, Kigoma
 Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wlbrod Slaa akiwa na Wananchi wa Kijiji cha Kitanga, Kigoma.Picha na Chadema
----
Pamoja na Mbinu Chafu za Kutaka Kuvuruga Mkutano wa Chadema Kasulu Uliokuwa Unahutubiwa na Dr Slaa, lakini wananchi wengi wa Kasulu walijitokeza kumsikiliza Dr Slaa na kufurahishwa na hotuba yake iliyobeba maneno ya kuwapa Matumaini. 
 
 Kulikuwa na kikundi cha Vijana wapatao kumi wenye mabango ambayo yaliandaliwa mahsusi ili yatumike kuvuruga mkutano huo lakini mbinu zao chafu zimeshindikana. Ili kuzima mipango yao michafu vijana hao walipewa fursa ya kukaa mbele na mabango yao yenye ujumbe wa kuwaponda viongozi wa Chadema.
 
 Vijana hao walipewa fursa hiyo ili kuonyesha kwamba Chadema kinaendeshwa kwa Demokrasia ya kumruhusu mwanachadema yeyote kutoa mawazo yake anayopenda ili kudumisha Demokrasia ndani ya Chama.

No comments:

Post a Comment