Makamu Mkuu wa Chuo KIkuu cha Bagamoyo (UB), Profesa Costa Ricky
Mahalu
----
MAKAMU Mkuu wa Chuo KIkuu cha Bagamoyo (UB), Profesa Costa Ricky
Mahalu anawatangazia mahafali ya kwanza ya kihistoria ya chuo hicho,
yatakayofanyika Jumamosi Desemba 7 mwaka huu, Saa nne asubuhi katika
Makumbusho ya Taifa karibu na Chuo Cha Usimamizi wa Fedha(IFM), Dar es
Salaam.
Profesa Mahalu aliyasema hayo leo katika mkutano wake na waandishi
wa habari uliofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya Chuo hicho,
Mikocheni B kwa Warioba, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa
Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Mohammed Gharib
Bilal.
Profesa Mahalu alisema chuo hicho kilianzishwa rasmi miaka miwili
na miezi mitatu iliyopita ambapo hadi sasa ina jumla ya wanafunzi zaidi
ya 850. Kwani wakati kilipoanzishwa mwaka 2011 chuo kilianza na
wanafunzi wa 65.Hadi sasa wana jumla ya koleji nne , koleji ya kwanza ni
ya Sheria, Ualimu, Sayansi Uchumi na sayansi ya Menejimenti.
Hata hivyo alitoa wito kwa waandishi wa habari wote nchini waone
wakati umefika sasa wakuanza kupenda kusoma fani ya sheria kwani wasomi
wa sheria na jamii imekuwa ikishuhudia baadhi ya habari zinazohusu
masuala ya kisheria kama habari za mahakamani zikilizipotiwa
hisivyosahihi na baadhi ya waandishi wa habari na kuongeza kuwa endapo
waandishi wengi wa habari waamue kusoma sheria wangeondokana na tatizo
hilo la kutokufahamu vyema kuripoti habari zinazohusu masuala ya
kisheria.
Aidha alisema tayari waandishi wa habari za mahakamani wawili
nchini wameishajiunga katika chuo hicho na wanasoma kozi ya shahada ya
sheria na kwamba chuo kinashuhudia mabadiliko makubwa sana ya uandishi
wenye radha ya kisheria unaonandikwa na waandishi hao katika vyombo vyao
vya habari kwasababu wanasoma sheria.
Mwisho
No comments:
Post a Comment